Umoja wa vijana wa klabu ya soka
ya Yanga ya jijini Dar es Salaam leo wamekutana katika makao makuu ya klabu
hiyo ili kujadili mstakabali wa timu yao pamoja na usajili wa msimu ujao wa
ligi kuu soka Tanzania bara.
Mkutano huo pia umejadili
hatma ya mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga, usajili wa msimu ujao pamoja
na mambo yaliyojitokeza kwenye mkutano ulioitishwa katikati ya wiki na Nchunga
klabuni hapo.
Mwenyekiti wa vijana wa klabu
hiyo Bakili Magele amesema yeye pamoja na vijana wenzie wataendelea na msimamo wao wa kumtaka Nchunga ajiuzuru Pamoja
na kamati ya utendaji ya klabu hiyo.
Baadhi ya vijana na wafurukwa wa Yanga wakapaza sauti zao na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kuachia ngazi ikiwa ni pamoja na kamati ya utendaji ya Yanga.
Katika maoni yao wanchama
wamelalamikia uongozi uliopo madarakani kwa kushindwa kuitisha mikutano mkuu
jambo ambalo ni kinyume na katiba ya Yanga.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment