AIRTEL YAZINDUA SUPA 5.
Kampuni ya simu za mkononi ya airtel imezindua huduma mpya
za mawasiliano kwenye mtandao huo ambapo sasa mteja wa kampuni hiyo ataweza
kupata huduma 5 za mawasiliano kwa wakati mmoja.
Kuzinduliwa kwa huduma hizo kutapunguza gharama za
mawasiliano kwa wateja wa kampuni hiyo kwa zaidi ya nusu huku huduma nyingine
zikitolewa bure.
Huduma zilizozinduliwa chini ya mpango huo ni Internet,
kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kupiga simu, punguzo la hadi bure kwa kupiga
simu usiku na kutumia internet bure wakati wa usiku.
Jackson Mbando ni meneja mawasiliano wa Airtel amesema faida zitokanazo na huduma hiyo ni kubwa na hivyo kuwataka wateja wa kampuni yao kutuzitumia ili wapate unafuu wa kutumia mawasiliano.
Huduma zinazoweza kupatikana ni pamoja na kuongea kwa Nusu shilingi kwa sekunde siku nzima kwa marafiki wa Airtel. Kuongea kwa robo shilingi kwa sekunde siku kucha Airtel kwenda Airtel. SMS 200 bure baada ya kutuma SMS kumi kwa kulipia shilingi 30 kwa SMS.Kuperuzi Internet Bure usiku mzima na Kufungua na kuperuzi Facebook Bure.
Kuzinduliwa kwa huduma hiyo kumelenga kupunguza bei ya
mawasiliano kwa wateja wa kampuni hiyo na pia kurahisisha matumizi ya internet.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment