Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha
wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi
Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Akitangaza
kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema
uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora
wake.
Wachezaji
walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius
Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris
(Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri
Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo
ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas
Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho
Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji
ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan
Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP
Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco
(Azam).
Stars
inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla
kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment