Kampuni ya
bia Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Grand Malt wamefanya tamasha la
michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu linalojulikana kama Excel Grand Malt lenye
lengo la kuhamasisha michezo baada ya masomo.
Tamasha hilo
limejumuisha michezo mablimbali ikiwemo mpira wa miguu, kikapu, kuvuta kamab
pamoja na pool table na kushuhudia mshindi akijinyakulia kitita cha
shilingi
laki 5.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa tamasha hilo meneja masoko wa TBL Fimbo Butala
amesema kuwa kwa kupitia kinywaji hicho watazunguka mikoa yenye vyuo vya elimu
ya juu ili kuhamasisha michezo vyuoni.
Nao baadhi
ya wanafunzi walioshirikikatika michezo mbalimbali wamesema kuwa ingawa
kulikuwa na mvua lakini ushindani umeonekana baina ya washiriki hao.
Bonanza hilo
litakuwa likifanyika kila mkoa kwa kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya
mikoa husika ili kuhamasisha michezo baada ya muda wa masomo kwa wanafunzi hao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment