MASHINDANO YA NETBALI AFRIKA YAMALIZIKA MALAWI MABINGWA TENA
Timu ya Taifa ya mpira wa
pete Taifa Queens imefanikiwa kupata tiketi ya kucheza michuano ya viwango vya dunia
baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Botswana na kushika nafasi ya pili katika
fainali za Afrika zilizomalizika jana jijini DSM.
Malkia hao wa Tanzania
wameshika nafasi hiyo baada ya kuishushia kipigo cha mabao 32 kwa 23 Botswana
katika mchezo mkali uliochezwa kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Mchezo huo uliokuwa wa mwisho
katika michuano hiyo ulilazimika kuahirishwa kutoka saa NANE mchana hadi saa
MOJA usiku baada ya kushindwa kuchezwa katika viwanja vya nje kutokana na mvua
kubwa uliyonyesha mfululizo jijini DSM.
Katika hali ya kustaajabisha…uwanja
wa ndani nako mambo hayakuwa shwari kabisaaa…pale ambapo mvua iliamua kuwafuata
wachezaji na kuharibu ladha yote ya mchezo,ikiwa ni pamoja na juhudi za
makusudi za mwamuzi wa mchezo huo na baadhi ya viongozi kushiriki zoezi la
kupiga deki uwanja….
Hii inakuwa mara ya kwanza
kwa Taifa Quens kukamata nafasi hiyo na sasa imepanda viwango kutoka vya Afrika hadi Dunia.
Mgeni rasmi katika mchezo huo
Mke wa Makamu wa Rais Aisha Bilal aliyeambatana na mke wa Waziri Mkuu Tunu
Pinda amewakabidhi wachezaji wa Taifa Queens kombe la ushindi wa pili na
mabingwa wapya wa michuano hiyo Malawi ambao wametetea ubingwa wao,na Zambia
ambao wameshika nafasi ya tatu.
Nchi ambazo zimeshiriki
michuano hiyo ni Lesotho, Zambia, Malawi ,Botswana, Zimbabwe na mwenyeji
Tanzania.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment